Masuala ya Kisheria na Utambuzi wa Hati (Legal & Notarial Services)
Ubalozi hauhusiki na utoaji wa ushauri wa kisheria lakini unaweza ukasaidia upatikanaji wa orodha ya Wanasheria waliopo China na nchi nyingine za uwakilishi. Hata hivyo, orodha hiyo haitajumuisha mapendekezo kuhusu Mwanasheria au Kampuni yeyote.
Huduma za Utambuzi wa Hati (Notarial services) kama vile utambuzi wa hati za kusafiria, uraia na vyeti; na viapo (Consular declarations, oaths, affirmations, affidavits, statutory declarations, certified true copies and witnessing of signatures on documents), hizo zinaweza kutolewa Ubalozini.
Ndoa
Watanzania wanaopanga kuoana nchini China, chini ya Sheria za Tanzania, wanaweza kufanya hivyo mara baada ya kukamilisha masharti muhimu yakiwemo: Kupata barua kutoka kwa wazazi wa pande zote mbili na Serikali za Mitaa wanapoishi zikionyesha kwamba wazazi wameridhia na kwamba mhusika bado hajaoa/ hajaolewa. Kwa mujibu wa Sheria, baada ya kukamilisha hayo, Balozi anaruhusiwa kufungisha Ndoa hiyo.
Kwa Watanzania wanaopanga kuoana nchini China, chini ya Sheria za China, wanashauriwa kuwasiliana na Ofisi zinazohusika na Usajili wa Ndoa kwani zinatofautiana kwa masharti na utaratibu unaotakiwa kufuatwa. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Ofisi ya Usajili wa Ndoa hapa Beijing kwa simu Na: 010-65008322 or 010-65008002 au kuwatembelea katika ofisi zao ziliyopo Liu Li Tun Dao Jia Yuan Bld. Na. 6, Wilaya ya Chaoyang, Beijing. Kwa wale waliopo nchini Tanzania wanashauriwa kuwasiliana na Ubalozi wa China uliopo Dar es Salaam kabla ya kuja nchini China kwa shughuli hizo za ndoa.
Dharura
Kitengo hiki cha masuala ya “Consular” kinatoa huduma za dharura masaa 24 kwa Watanzania wenye matatizo. Kwa msaada baada ya masaa ya kazi wasiliana na Afisa mhusika kwa kupitia. Ubalozi
Kwa wale waliopo nchini Tanzania, wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao watasaidia kuwasiliana na Ubalozi wetu.